Inatafuata...


Online Passport Application        

Hii ni huduma mpya inayomuwezesha muombaji kujaza Fomu ya Maombi ya Pasipoti kwa njia ya Kielektroniki kutokea popote alipo, Baada ya kujaza fomu hiyo mtandaoni
na kuambatisha picha yake kama atakavyoelekezwa mtandaoni, atatakiwa kuichapisha (Print) fomu hiyo na kufika nayo katika Ofisi ya Uhamiaji iliyo karibu naye
kwa ajili ya kushughulikiwa maombi yake ya Pasipoti.

Huduma hii itamwondolea usumbufu wa kwenda ofisini kuchukua fomu ya maombi ya pasipoti, na badala yake ataipata na kuijaza fomu hiyo mtandaoni. Aidha, itasiaidia
katika kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu na baadae kumwezesha mteja kufuatilia hatua lilipofikia ombi lake kwa njia ya mtandao.