Latest Events

TAARIFA KWA UMMA

logo

TAARIFA KWA UMMA

Kuna taarifa zinazosambazwa  katika  mitandao ya kijamii ambazo zimezua  taharuki na sintofahamu katika jamii. Taarifa hizo zinadai kwamba  Watanzania waliopata pasipoti zao Tanzania Bara wanazuiliwa kusafiri kwenda nje ya nchi kupitia Zanzibar.

Idara ya Uhamiaji inakanusha taarifa hizo kwamba sio za kweli na ni upotoshaji unaofanywa makusudi na watu wenye dhamira mbaya ya kuichafua taasisi na nchi yetu kwa ujumla.

Hali halisi iliyopo ni kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezuia kuondoka kiholela kwa Watanzania hususan wasichana wanaokwenda kufanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati. Hii imefanyika kutokana na matukio mengi ya unyanyasaji pamoja na kukosa haki zao wanapokuwa wanafanya kazi katika nchi hizo. Mawakala wasiowaaminifu waliokuwa wakiwasafirisha Watanzania hao  walibadili mbinu na kuanza kuwasafirisha wasichana hao kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) uliopo Zanzibar bila ya kufuata taratibu zinazotakiwa.

Baada ya kubainika kwa mbinu ya mawakala  hao udhibiti uliongezwa katika kituo cha AAKIA ili kuhakikisha wasichana hao wanasafiri kwenda nje ya Tanzania kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.  

Raia yeyote wa Tanzania  ambae amekidhi matakwa ya kisheria ana haki ya kusafiri kwenda  nje ya nchi kupitia kituo chochote cha mpakani au uwanja wa ndege uliopo popote    nchini bila ya kujali pasipoti yake imetolewa eneo  gani la Tanzania.

Wananchi wanatakiwa kuzipuuza na kuacha kuzisambaza taarifa hizo,  Aidha uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini walio anzisha na  wanaosambaza uzushi huo na uchunguzi huo utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO,

IDARA YA UHAMIAJI,

MAKAO MAKUU.

16 MACHI, 2018.

News and Events

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA Kuna taarifa zinaz...

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA (MPYA)

Facebook Fan Page

Visitors Counter

TodayToday512
This WeekThis Week10816
This MonthThis Month34486
All DaysAll Days611248
Visitors Online 15