Latest Events

WAGENI WOTE WENYE VIBALI VYA UKAAZI(MPYA)

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

IDARA YA UHAMIAJI

 

 

15

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WAGENI WOTE WENYE VIBALI VYA UKAAZI WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA OFISI ZA UHAMIAJI ZILIZOPO KATIKA MAENEO WANAYOISHI NA KUFANYIA KAZI WAKIWA NA VIBALI VYAO.


Idara ya Uhamiaji inapenda kuwafahamisha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote wanaoishi na kufanya kazi nchini kwamba wanatakiwa kuripoti na kuwasilisha taarifa za anuani zao zikiwemo na mabadiliko katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo katika maeneo wanayoishi na kufanya kazi katika kipindi cha siku thelathini 30 tangu kutolewa kwa taarifa hii.Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kuhuisha taarifa na kumbukumbu za Wageni wakaazi ambao baadhi yao wamehama maeneo yao ya awali na kuhamia sehemu nyingine na linafanyika kwa mujibu wa Kanuni ya 29 (1), (2) na 30 za Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 na Marekebisho yake ya Mwaka 2016, chini ya Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 Rejeo la Mwaka 2002.Aidha, ieleweke kwamba kutokufanya hivyo ni kosa kisheria chini ya Kanuni ya 29 (3) na 37 ya Kanuni za Uhamiaji za Mwaka 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2016 chini ya sheria ya uhamiaji sura 54 rejeo la mwaka 2002.


Imetolewa na


SAMWEL RHOBBY MAGWEIGA

KAMISHNA WA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA MIPAKA,

MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI,

05 OKTOBA, 2017.

 

News and Events

TAARIFA KWA UMMA

UZINDUZI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI M...

TAARIFA KWA UMMA

WAGENI WOTE WENYE VIBALI VYA UKAAZI(MPYA...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZA...

Facebook Fan Page

Visitors Counter

TodayToday182
This WeekThis Week117
This MonthThis Month22996
All DaysAll Days299881
Visitors Online 21