Latest Events

TAARIFA KWA UMMA

UZINDUZI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI MTANDAONI

(ONLINE PASSPORT APPLICATION FORM) 

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

                                                      IDARA YA UHAMIAJI      

TAARIFA KWA UMMA

KUZINDULIWA KWA HUDUMA YA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI MTANDAONI (ONLINE PASSPORT APPLICATION FORM)

Idara ya Uhamiaji inapenda kuutangazia umma kuwa imezindua rasmi huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form). Huduma hii inapatikana katika tovuti ya Idara kupitia link ifuatayo: https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ na itaanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 07 Agosti, 2017.

Kufuatia kuzinduliwa kwa huduma hii, waombaji wote wa pasipoti wanashauriwa kuzijaza fomu hizo mtandaoni, Kisha kuzichapisha (Printing) na kuziwasilisha katika Ofisi za Uhamiaji.

Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo.

Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ambayo ni  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao.

Taarifa zaidi kuhusu huduma hii zitaendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Imetolewa na:

KITENGO CHA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,

04 AGOSTI, 2017.

News and Events

TAARIFA KWA UMMA

UZINDUZI WA FOMU YA MAOMBI YA PASIPOTI M...

TAARIFA KWA UMMA

WAGENI WOTE WENYE VIBALI VYA UKAAZI(MPYA...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZA...

Facebook Fan Page

Visitors Counter

TodayToday201
This WeekThis Week136
This MonthThis Month23015
All DaysAll Days299900
Visitors Online 22