• 31 januari, 2018
    31 januari, 2018

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha Pasipoti Mpya ya Kielektroniki ya Tanzania.

  • 9 Septemba, 2020
    9 Septemba, 2020

    Wasafiri wakipata huduma katika kaunta za uhamiaji, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume -Zanzibar.

  • 09 Disemba, 2021
    09 Disemba, 2021

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha Nishani ya Miaka 60 ya Uhuru CGI Dkt. Anna Makakala ikulu Dsm 09 Disemba 2021

  • 09 Disemba,2021
    09 Disemba,2021

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassa akikagua Gadi ya Uhamiaji wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Uhuru 09 Disemba 2021 Dsm

  • 12 Januari, 2022
    12 Januari, 2022

    Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt Hussein Mwinyi akikagua gadi ya Uhamiaji wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar  2022

  • 15 Agosti, 2022
    15 Agosti, 2022

    Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  akipanda mti wa kumbukumbu katika Chuo cha Uhamiaji cha Rapheal Kubaga kilichopo Boma Kichakamiba mkoani  Tanga. Mhe. Rais alikuwa hapo kwa ajili ya kuzindua chuo hicho pamoja na kufunga mafunzo ya awali kwa askari wa Uhamiaji.

Kigoma, Tanzania

Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma imewakamata wahamiaji haramu 73, ambapo 56 wamethibitika kuwa wahamiaji haramu na 17 uchunguzi wa uraia wao unaendelea na wote hawa  wanashikiliwa  kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mapema wiki hii Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (ACI) Augustino Matheo amesema Idaa ya uhamiaji mkoa imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu hao kutokana na kufanyika doria na misako mbalimbali iliyofanyika tarehe 03 Machi 2021.

ACI Matheo amefafanua zaidi kwamba waliokamatwa nia raia 51 wa nchi jirani ya Burundi, raia wa Kongo DRC 04, raia wa Rwanda 01 na Wanaodai ni raia wa Tanzania17 ambapo uchunguzi unaendelea ili kubaini uraia wao.

“Wahamiaji haramu hawa wamekamatwa katika mwalo wa ziwa Tanganyika eneo la Kibirizi mkoani Kigoma, Katika maelezo yao tumegundua walikuwa wanajishughulisha na uvuvi” alisema ACI Matheo

Aidha ametoa tahadhari kwa mwananchi yeyote atakayekutwa amewahifadhi wahamiaji haramu katika nyumba yake au akiwa anawasafirisha kwenye gari (chombo cha usafiri) atachukuliwa hatua kali za kisheria zikiwemo kushitakiwa mahakamani, nyumba au chombo alichokua anakitumia kusafirishia au kuwahifadhia wahamiaji haramu vinaweza kutaifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kwamba tayari hatua zimechukuliwa mara baada ya kukamilisha  taratibu zote watafikishwa mahakamani ka kosa la kuingia nchini kinyume na sheria za nchi.

“Wale wote wanaoingia nchini kupitia vipenyo visivyo rasmi (Panya Roots) tutawakamata wote, vilevile tunawaomba wananchi watupe ushirikiano pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili tuwabaini wahamiaji haramu na mtandao wao” alisema

Onyo limetolewa kwa Mkoa wa Kigoma kwamba Mkoa huo sio kichaka wala njia au maficho ya wahamiaji haramu kupitia kwenda sehemu zingine za nchi, kwani Idara imejipanga kidete kuwezesha na kudhibiti uingiaji na utokaji wa watu kupitia utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo ili kulinda usalama wa Taifa na kukuza maendeleo ya kiuchumi.

Dr. Anna P. Makakala

Commissioner General of Immigration

News and Events

KUITWA KWENYE MAFUNZO - MARCH, 2024

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia Vijana waliofaulu usaili na kuchaguliwa, kujiunga na Chuo cha Uhamiaji Raphael Kubaga kilichopo Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, kuwa wanatakiwa kuripoti tarehe 03 Aprili, 2024...

TAARIFA KWA UMMA 02 April, 2024

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji; ambao walitakiwa kuripoti kwenye mafunzo katika Chuo cha Uhamiaji cha Raphael Kubaga kilichopo mkoani Tanga tarehe 03 Aprili,...

« »