Uhamiaji Zanzibar Yachangia Damu Kwa Hiari

Zanzibar

Idara ya Uhamiaji Zanzibar mapema wiki hii imefanya zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari kwa Maafisa, Askari na watumishi raia wa Idara ya Uhamiaji wanaofanya kazi Zanzibar, zoezi ambalo limefanyika Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar.

Kaimu Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar DCI Nassra Juma Mohamed amewakaribisha waratibu kutoka Wizara ya Afya kitengo cha damu salama na kuwaahidi ushirikiano mzuri katika kufanikisha zoezi hili.

DCI Nassra amewashajihisha watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuchangia damu na kueleza kwa ufupi umuhimu wa suala la uchangiaji wa damu kwa watumishi.

Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya kuchangia damu Zanzibar Bwana Bakari Hamad Magarawa, amefafanua kuwa zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari ni kawaida kufanyika katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuhamasisha watumishi kujitokeza kuchangia damu kwa wingi, kwani hakuna tatizo la kiafya linalotokana na kuchangia damu.

Aidha amewaomba watumishi kuanzisha klabu ya uchangiaji damu “donor club” itakayosaidia mtumishi yoyote kufaidika endapo atapata tatizo la upungufu wa damu.

Bwana Magarawa ameendelea kueleza faida nyengine ya uchangiaji wa damu kwa watumishi ikiwa ni pamoja na mtu kupewa kadi ya uanachama ya kuchangia damu ambayo itamsaidia yeye na familia iwapo itapata tatizo la upungufu wa damu.

Jumla ya watumishi 35 wamejitokeza katika zoezi hilo la uchangiaji damu salama na kufanya zoezi la uchangiaji damu salama kufanikiwa katika kiwango kizuri.

News and Events

Uhamiaji Zanzibar yatoa mafunzo ya E-visa kwa wadau wa utalii na kampuni za usafirishaji

2021-03-19
Uhamiaji Zanzibar yatoa mafunzo ya E-visa kwa wadau wa utalii na kampuni za usafirishaji

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu ameongoza semina ya viza za kielektroniki kwa wadau mbali mbali wa utalii na kampuni za usafirishaji (ground handler) mapema mwaka huu katika ukumbi...

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala ahudhuria safari ya mwisho ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

2021-04-19
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala ahudhuria safari ya mwisho ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala mapema wiki hii alihudhuria ibada ya mwisho na mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John...

Uhamiaji Zanzibar Yachangia Damu Kwa Hiari

2021-04-19
Uhamiaji Zanzibar Yachangia Damu Kwa Hiari

Zanzibar Idara ya Uhamiaji Zanzibar mapema wiki hii imefanya zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari kwa Maafisa, Askari na watumishi raia wa Idara ya Uhamiaji wanaofanya kazi Zanzibar, zoezi...

Habari Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia Bunge

2021-05-09
 Habari Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia Bunge

Habari Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan Mapema leo hii amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa...

« »