Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala ahudhuria safari ya mwisho ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala mapema wiki hii alihudhuria ibada ya mwisho na mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufulikatika uwanja wa Magufuli na makaburi ya familia yaliyopo Chato, Mkoani Geita.

Majira ya saa 10:50 jioni jeneza lenye mwili wa Hayati Magufuli lilishushwa kaburini na kufuatiwa na tukio la ndugu, jamaa na marafiki kuweka mchanga.

Hayati Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 61.

Shughuli ya mazishi imeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, mke wa marehemu Mama Janeth Magufuli, marais wastaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, viongozi wa dini na siasa.

Mbali na hao shughuli hiyo pia imeshuhudiwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafamilia, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mabalozi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makamishna wa Uhamiaji, wasanii pamoja na baadhi ya wakazi wa Chato na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.

Shughuli ya maziko ilifanyika Kijiji cha Mlimani wilayani Chato Mkoa wa Geita katika makaburi ya familia ilihusisha watu wachache wakiwemo viongozi wa Serikali, wastaafu na familia yake.

News and Events

Uhamiaji Zanzibar yatoa mafunzo ya E-visa kwa wadau wa utalii na kampuni za usafirishaji

2021-03-19
Uhamiaji Zanzibar yatoa mafunzo ya E-visa kwa wadau wa utalii na kampuni za usafirishaji

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu ameongoza semina ya viza za kielektroniki kwa wadau mbali mbali wa utalii na kampuni za usafirishaji (ground handler) mapema mwaka huu katika ukumbi...

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala ahudhuria safari ya mwisho ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

2021-04-19
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala ahudhuria safari ya mwisho ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini CGI Dkt. Anna Makakala mapema wiki hii alihudhuria ibada ya mwisho na mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John...

Uhamiaji Zanzibar Yachangia Damu Kwa Hiari

2021-04-19
Uhamiaji Zanzibar Yachangia Damu Kwa Hiari

Zanzibar Idara ya Uhamiaji Zanzibar mapema wiki hii imefanya zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari kwa Maafisa, Askari na watumishi raia wa Idara ya Uhamiaji wanaofanya kazi Zanzibar, zoezi...

Habari Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia Bunge

2021-05-09
 Habari Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia Bunge

Habari Picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan Mapema leo hii amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taifa...

« »